Machapisho

DANIEL; ATOA MAKALA YA NDOA

UKUMBI WA SHWANGWE Katika kufurahia na kumshukuru Mwenyezi Mungu .Mr Daniel ameandika makala ili kuisa jamii mambo muhimu kwa wanandoa. Makala hiyo yenye kichwa habari: UKIIGIZA MAISHA NDOA ITAKUSHINDA. Bwana Daniel ameongelea mambo mengi mazuri sana katika mahusiano. Makala hii inapatikana katika gazeti la Mtanzania la tarehe 3 september 2017

TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI

Picha
TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI KIGAMBONI, DAR ES SALAAM Vijana kutoka chuo cha Munister nchini Ujerumani, wametembelea kituo cha Taasisi ya kijamii ya kuendeleza Vijana na Kinamama katika ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo kigamboni Dar es salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira. Vijana zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo usafi, kushiriki mafunzo ya ushonaji nguo katika kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazowakabili kinamama. Wageni kutoka "Pamoja 5th Generation" (Munster university & Mwl nyerere memorial academy) na wenyeji wao kutoka TaGEDO katika picha ya pamoja Wageni kutoka Pamoja "5th Generation" (Munster university & Mwl nyerere memorial academy) wakishiriki kazi mbali mbali TaGEDO