TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI

TaGEDO YAPATA UGENI KUTOKA UJERUMANI

KIGAMBONI, DAR ES SALAAM

Vijana kutoka chuo cha Munister nchini Ujerumani, wametembelea kituo cha Taasisi ya kijamii ya kuendeleza Vijana na Kinamama katika ujasiriamali hapa nchini (TaGEDO) kilichopo kigamboni Dar es salaam, na kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo kusafisha mazingira.
Vijana zaidi ya 20 walishirikiana na vijana wenzao kutoka TaGEDO na kufanya shughuli mbali mbali ikiwemo usafi, kushiriki mafunzo ya ushonaji nguo katika kituo hicho na baadaye ulifanyika mjadala wa kubadilishana uzoefu katika mafanikio na changamoto zinazowakabili kinamama.
Wageni kutoka "Pamoja 5th Generation" (Munster university & Mwl nyerere memorial academy) na wenyeji wao kutoka TaGEDO katika picha ya pamoja

Wageni kutoka Pamoja "5th Generation" (Munster university & Mwl nyerere memorial academy) wakishiriki kazi mbali mbali TaGEDO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

DANIEL; ATOA MAKALA YA NDOA